Christopher Mtikila atangaza kuwania mgombea binafsi wa Urais Tanzania
3 Machi 2010Matangazo
Wagombea wamekuwa wakijiandaa kwa uchaguzi huo na hata chama
kipya cha jamii kimepata usajili wa muda mwanzoni mwa wiki hii. Kwa
upande mwengine, suala la kuruhusiwa mgombea binafsi kushiriki katika
uchaguzi mkuu bado linaendelea kuzusha mitazamo tofauti. Kutokana na
hilo, Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia, Christopher Mtikila,
ametangaza kuwa hata chama chake kisipomteua kuwawakilisha katika
uchaguzi, yeye atawania wadhifa wa rais kama mgombea binafsi.
Atafanikiwa? Mwandishi wetu wa Dar es salaam, Christopher Buke,
alikutana na Christopher Mtikila na haya ndiyo aliyomulezea
Mwandishi: Thelma Mwadzaya
Mhariri: Othman Miraji