1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Champions league:Schalke 04 kuvaana na Valencia

15 Februari 2011

Ligi ya mabingwa barani Ulaya kutimua vumbi hii leo.

https://p.dw.com/p/10HUc
Wachezaji wa Schalke 04 wakiwa mazoeziniPicha: picture-alliance/dpa

Katika mechi za leo,Tottenham Hotspur inarejea katika uwanja wa

San Siro kupambana na AC Milan, huku Valencia wakiwa wenyeji wa Schalke 04.

Mara ya mwisho wa Tottenham Hotspur kucheza San Siro ilichapwa mabao 4-3, ambapo ikiwa nyuma kwa mabao 4-0 iliweza kupachika mabao 3 na katika mechi ya marudiano ikawafunga wataliano hao kwa mabao 3-1 na kuongoza katika kundi lao.

Nayo Schalke 04 inategemea kuonesha upinzani wa hali ya juu kwa wenyeji wao Valencia, kutokana na kiwango ilichoonesha katika hatua ya makundi, ambapo iliongoza kutoka katika kundi lake.

Kesho ligi hiyo itashuhudia mechi kali kati ya Arsenal na Barcelona mjini London, pambano ambalo linachukuliwa kama marudio ya robofainali ya michuano hiyo mwaka jana pamoja na fainali ya mwaka 2006, mechi ambazo zote Barcelona ilishinda.

Mwandishi:Aboubakary Liongo/Reuters

Mhariri:Mohamed Abdulrahman