Champions League:Bayern kukutana na Inter Milan | Michezo | DW | 17.12.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

Champions League:Bayern kukutana na Inter Milan

Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA limetangaza ratiba ya ligi ya mabingwa hatua ya mtoano pamoja na michuano ya UEFA.

default

Kocha wa Bayern Munich Loius van Gaal

Katika ligi ya mabingwa timu 16 zitashuka dimbani kuwania tiketi ya robofainali, ambapo miongoni mwa mechi hizo ni ile kati ya Bayern Munich na mabingwa watetezi Inter Milan.

Timu hizo zilikutana katika fainali iliyopita ya michuano hiyo, iliyoshuhudia Inter ikiichapa Bayern mabao 2-0 na kutwaa ubingwa. Wakati huo Inter ilikuwa chini ya Jose Morinho ambaye kwa sasa kaupeleka uchawi wake Madrid katika klabu ya Real Madrid.

Morinho kapangwa kuwaongoza vijana wake dhidi ya Lyon, huku Schalke 04 ikiumana na Valencia. Barcelona inayopigiwa upatu kutwaa ubingwa itapambana na Arsenal, ilhali AC Milan imepangwa kuumana na Tottenham Hotspur.

Ratiba hiyo pia inaonesha AS Roma imepangwa kupambana na Shakhtar Donetsk, nayo Chelsea ikionekana kupata mteremko kwa kupangwa dhidi ya FC Copenhagen. Marseille ya Ufaransa itakuwa na kibarua mbele ya Manchester United. Mechi hizo zitachezwa Februari mwakani.

Katika michuano ya UEFA, Stuttgart inayopepesuka katika ligi ya Bundesliga imepangwa kuumana na Benfica ya Ureno, huku Bayer Levekusen ikipangwa na Metalist Kharko ya Ukraine.

Mwandishi:Aboubakary Liongo

Mhariri:Josephat Charo

 • Tarehe 17.12.2010
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/QeiD
 • Tarehe 17.12.2010
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/QeiD