1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Cairo:Rice akutana na Mubarak

25 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCFO

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Condoleezza Rice amekua na mazungumzo na Rais Husni Mubarak wa Misri mjini Cairo, kuhusu kuufufua mwenendo wa amani ya mashariki ya kati. Mazungumzo yao yaligubikwa na matamshi ya bibi Rice hapo awali kuukosoa mpango wa marekebisho ya katiba ya Misri. Kesho wamisri watapiga kura ya maoni juu ya marekebisho hayo, ambayo jumuiya za haki za binaadamu zimeyaita “hatua moja nyuma.” Baadae Bibi Rice ataonana na Rais wa wapalestina Mahmoud Abbas, kabla ya kuelekea Israel na Jordan. Hii ni ziara ya nne ya waziri huyo wa mambo ya nchi za nje wa Marekani katika mashariki ya kati, baada ya kipindi cha miezi mingi.