CAIRO:Misri yaimarisha mpaka wake na Gaza | Habari za Ulimwengu | DW | 21.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

CAIRO:Misri yaimarisha mpaka wake na Gaza

Misri inaimarisha ulinzi katika mpaka wake na Ukanda wa Gaza huku ikilaumu nchi ya Iran kwa kuhatarisha usalama nchini mwake baada ya wapiganaji wa Chama cha Hamas kuteka eneo hilo.Polisi wa ziada wanashika doria katika eneo la mpakani ili kudhibiti wakimbizi kutoka Ukanda wa Gaza.

Kulingana na Waziri wa mambo ya nje wa Misri Ahmed Abul Gheit Iran inaunga mkono chama cha Hamas kuteka Ukanda wa Gaza.Vyama vya hamas na Fatah vinazozana katika eneo la Palestina tangu wiki jana na kusababisha vifo vya watu 110.

Iran ilivunja uhusiano wake na Misri baada ya kufikia makubaliano ya amani na Israel mwaka 79.Misri inakashifu utekaji wa Gaza uliofanywa na Hamas na kuunga mkono serikali ya dharura ya Rais Mahmoud Abbas iliyoko katika Ufukwe wa Magharibi.Misri aidha imehamisha ubalozi wake kutoka mji wa Gaza hadi Ramallah ambako ndio makao makuu ya serikali mpya ya Mahmoud Abbas.

Kundi la Hamas lilundwa mwaka 87 na wafuasi wa Muslim Brotherhood ambacho ni chama kikubwa cha Upinzani nchini Misri.Hatua ya chama cha Hamas kuteka eneo la Ukanda wa Gaza imesababisha takriban watu 400 kuomba hifadhi nchini Misri wengi wao wafuasi wa Rais Mahmoud Abbas.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com