Cairo. Umoja wa mataifa ya Kiarabu wataka majeshi ya yote ya kigeni kuondoka Iraq. | Habari za Ulimwengu | DW | 05.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Cairo. Umoja wa mataifa ya Kiarabu wataka majeshi ya yote ya kigeni kuondoka Iraq.

Jumuiya ya mataifa ya Kiarabu imetoa wito kwa baraza la usalama la umoja wa mataifa kuweka muda ambao majeshi yote ya kigeni yataondoka kutoka Iraq.

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa mataifa ya Kiarabu wanaokutana mjini Cairo , wamesema kuwa muda huo uandikwe katika muswada wa azimio la umoja wa mataifa.

Wakati huo huo wameitaka serikali ya Iraq kuondoa sheria zote ambazo zinaruhusu kupewa upendeleo maalum kwa Washia na Wakurd. Wameongeza kuwa makundi yote ya wanamgambo wa Kishia yanapaswa kuvunjwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com