CAIRO : Msichana afariki kutokana na mafua ya ndege | Habari za Ulimwengu | DW | 26.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

CAIRO : Msichana afariki kutokana na mafua ya ndege

Msichana wa Misri mwenye umri wa miaka ya 15 amekufa kutokana na ugonjwa wa homa ya mafua ya ndege mjini Cairo ikiwa ni kifo cha pili kutokea baada ya siku nyingi.

Msichana huyo anatoka katika familia moja na mwanamke mwenye umri wa miaka 30 ambaye amefariki hapo Jumapili. Maafisa wa afya wa Misri wanasema watu hao waliokufa pamoja na wengine wawili ambao waliuguwa yumkini wakawa wameambukizwa kirusi cha ugonjwa huo kutoka kwa mabata walioko kwenye shamba la famila yao.

Misri iko kwenye njia kuu inayotumiwa na ndege wanaohama hama na imeshuhudia idadi kubwa ya kesi za homa ya mafua ya ndege ikitanguliwa na Indonesia na China.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com