Bush na bajeti yake | Matukio ya Kisiasa | DW | 06.02.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Bush na bajeti yake

Rais George Bush anakumbana na ubishi mkali kutoka kwa wademocrat na baadhi ya warepublikan juu ya mpango wake wa kutuma askari 21.500 zaidi nchini Irak jinsi ya kuugharimia mradi huo.

Bush na bajeti yake matatani

Bush na bajeti yake matatani

Vita vya Irak vilikuwa mada kubwa ya mabishano hapo jana mjini Washington.

Mjadala mrefu katika Baraza la senate kuhusu vita vya Irak hauwezi kuepukika licha ya juhudi za chama cha Republican cha rais George Bush kuutia munda- hii ni kwa muujibu wa chama cha Democrat.Wademocrat wameahidi kupata njia mwishoe kumfanya kila mjumbe wa Baraza la senate afahamike alichukua msimamo gain juu ya swali la Irak.

Mezani mbele ya Baraza hilo la senate ni azimio lisilomlazimisha rais Bush na linaloungwamkono na warepublican wengi na sehemu kubwa ya wademocrat litakalopinga hatua ya rais Bush ya kupelejka Irak askari 21,500 zaidi.

Rais anapaswa kusikia sauti ya bunge la marekani ili atambue anasimamia juu ya mguu mbovu na yuko peke yake-alkisema kiongoziwa chama cha democrat katika Senate Harry Reid.

Bush amesema askari hao zaidi wanahitajika kumtuliza shetani wa mapigano ya madhehebu ya shiia na sunni nchini Irak.Majadiliano kluhusu jinsi gani kusonga mbele na mjadalay juu ya azimio hilo yanatazamiwa kuendelea hii leo huku waziri wa ulinzi Robert Gates akienda Capitol Hill kutetea kwanini rais Bush anahitaji kitita cha dala bilioni 624.6 kwa ulinzi.

“Tumethibitisha na bunge la Congress linapaswa kusikiliza barabara kwamba bajeti hiyo itasawazishwa mnamo muda wa miaka 5 bila kubidi kupandisha kodi,bali kwa kuweka mezani ya matumizi.”

Hatahivyo, Rais Bush hana azma ya ya kupandisha kodi ambayo mwanzoni mwa kipindi chake cha utawala alipunguza kwa muda maalumu.

Alisema: “Kwa kutoza kodi ndogo tunakuza mapato katika hazina ya serikali.”

Adai Bush na hii ilimkasirisha mwenyekiti wa halmashauri ya bajeti kutoka chama cha democrat,seneta Kengt Conrad:

“Huo nitauita “ni mpango wa madeni wenye ujanja mwingi na usioshikamana kabisa na ukweli wa hali ya mambo.”Asema mjumbe wa chama cha upinzani cha democrat.

Kwa mfano, majeti ya wizara ya ulinzi itapanda hapo kwa kima cha 11%.Pekee kwa kugharimia vita vya Irak na Afghanistan ,rais Bush ameweka kando kima cha dala bilöioni 245-dala bilioni 100 kwa matumizi ya mwaka huu.

Ukihisabu pamoja na dala bilioni 70 ambazo tayari zimeshatumika ,huu utakua mwaka wa matumizi makubwa kabisa tangu kuanza kwa vile vita vilivyonadiwa dhidi ya “ugaidi”.

“usoni kabisa ni usalama wa wamarekani na kutoa fedha za kutosha kwa vikosi ili viweze kutekeleza jukumu lao.”Asema rais Bush.

Seneta Conrad wa chama cha upinzani cha Demokrat anashikilia msimamo wake ule ule kuwa Bush anawatia watu kitunga cha macho wasione mipango yake hasa.Kwani hasemi kile hasa anachoazimia kufanya.

 • Tarehe 06.02.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHKg
 • Tarehe 06.02.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHKg

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com