Bundesliga na Premier League uwanjani- | Michezo | DW | 21.09.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

Bundesliga na Premier League uwanjani-

Mwishoni mwa wiki hii Ligi zarudi uwanjani lakini Chelsea bila Jose Mourinho.Wanariadha wanyan'ganyia kitita cha dala milioni 3 huko Stuttgart na Marekani kusakata dimba Afrika Kusini.

Stuttgart-mabingwa uwanjani leo

Stuttgart-mabingwa uwanjani leo

Jose Mourinho hatakuwa mbali sana na uwanja wa Old Trafford,nyumbani mwa Manchester United pale klabu yake ya Chelsea alioiachamkono majuzi ikiwa na miadi kesho na mabingwa Manchester united.

Timu ya taifa ya Marekani itafunga safari yake ya kwanza kucheza na Bafana Bafana-Afrika Kusini hapo novemba,muda mfupi kabla FIFA kupiga kura ya jinsi timu 32 zitakavyoumana katika kombe lijalo la dunia 2010-la kwanza barani Afrika.

Ramadhan ali ananza lakini kwa kuwafunulia kawa la changamoto za mwishoni mwa wiki hii:

Baada ya nusu-finali ya kwanza jana ya kombe la Afrika la klabu bingwa-champions League kati ya Etoile du sahel ya Tunisia na Al Hilal ya Sudan,mjini Omduraman,kesho itakua zamu ya mabingwa Al Ahly ya Misri kujaribu kuitimua Al-Ittihad ya Libya mjini Tripoli ili kutwaa taji kwa mara ya 3 mfululizo.

Al-Merreikh ya Sudan inaweza nayo kukata tiketi ya finali ya kombe la shirikisho la dimba la Afrika ikiwa itaitimua nje Ismailia ya Misri mwishoni mwa wiki hii.Ikiwa Al-Merreikh itatamba na Kwara united ikiishinda timu nyengine ya Nigeria Dolphin,uamuzi timu gani 2 zitaibuka kileleni mwa kundi B utakatwa.Klabu hii ya omduraman ilijiimarisha karibuni kwa kujiunga nayo mlinzi wa zambia Elijah Tana na mbrazil Paulinho Roberto.

Hata katika kundi A mambo magumu:CS Sfaxien ya Tunisia ikiwa na pointi 7 iko mbele kwa pointi 1 tu kutoka TP Mazembe ya J.K.Kongo na Mamelodi ya afrika kusini.Mazembe na mamelodi kila moja lazima ishinde ili isonge mbele.

Marekani itafunga ziara yake ya kwanza Agfrika kusini,kituo cha kombe lijalo la dunia kucheza na wenyeji-Bafana Bafana hapo Novemba.Mpambano huo utatangulia kwa siku chache tu kura ya jinsi timu 32 zitakavyopambana katika duru za kwanza za Kombe la dunia 2010.Mapambano huo utachezwa Johannesberg,Nov.17 na utaania kombe la Mandela huko Ellis Park,uwanja utakaochezewa nusu-finali za kombe la dunia 2010.

Bundesliga –Ligi ya Ujerumani, inarudia uwanjani leo huku Schalke ikiwa na uchu mkubwa kutamba mebele ya Arminia Bielefeld.Jumamosi iliopita,Schalke ilitoka sare bao 1:1 na Bayern Munich na leo inahitaji ushindi mwengine tangu ule wa mabao 4:1 dhidi ya B.Dortmund.

Changamoto nyengine leo –Hamburg ina miadi na Nuremberg,Cottbus na Wolfsburg wakati hansa Rostock inaumana na Duisburg.Mabingwa Stuttgart wana kibarua kigomo katika mpambano wao na Werder Bremen.Bayern Munich inacheza na Karlsruhe,timu ya zamani ya kipa wao Oliver Kahn,alioichezea kwa miaka 7.

Jumapili, Hannover 96 itakamilisha duru hii kwa changamoto na Leverkusen.

Kesho Chelsea ilioachana mkono na kocha wake maarufu Jose Mourinho ina miadi na Manchester united katika changamoto za premier League.Na Mourinho ambae mashabiki wa Chelsea wamestushwa na kuondoka kwake, hatakuwa mbali na hapo kujua mpambano huo unamalizika vipi.

Ustadi wa kocha Mourinho uliwavutia akina Drogba,John Terry na hata frank Lampard na wote wamehuzunishwa na kuondoka kwake.Mashabiki wa Chelsea wameweka matanga hadi kesho ambapo ushindi tu mbele ya mabingwa Manchester ndio utakaomaliza kilio chao.

Riadha:

Msimu wa riadha 2007 unakamilishwa rasmi mwishoni mwa wiki hii mjini Stuttgart,kusini mwa Ujerumani:Mabingwa wa riadha wataondoka na vitita vikubwa vya fedha-wiki tu tangu wanariadha 2 Sanya Richards wa Marekani bingwa wa mita 400 na mrusi Yelena Isinbayeva anaeruka kwa upongoo kutoroka na kitita cha dala milioni 1 cha golden League mjini berlin.Stuttgart itagawa kitiota cha dala milioni 3.

Mshindi wa kila mchezo leo katika Daimler Stadium ataondoka na dala 30.000 huku mshindi wapili atajipatia dala 20.000 na watatu dala 10.000.Kiasi cha mabingwa 70 waliotamba katika mashindano ya dunia ya Osaka, wamekata tiketi za kushiriki Stuttgart kupitia pointi zao za ushindi.

 • Tarehe 21.09.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHb0
 • Tarehe 21.09.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHb0