Brussels.Uturuki yatakiwa kuongeza kasi ya mageuzi na kufikia muwafaka na Cyprus. | Habari za Ulimwengu | DW | 09.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Brussels.Uturuki yatakiwa kuongeza kasi ya mageuzi na kufikia muwafaka na Cyprus.

Kansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel ameitaka Uturuki kuongeza kasi ya mageuzi yake na kufikia masharti yaliyowekwa juu ya jirani yake Cyprus.

Kauli hii imekuja baada ya Kamisheni ya Umoja wa Ulaya, kutoa ripoti inayolaumu kuzorota kwa mageuzi ya kisiasa ya Uturuki tangu Umoja wa Ulaya ulipoanza mazungumzo na Uturuki mwaka mmoja uliopita, kuhusu takwa lake la kutaka kujiunga na umoja huo.

Kamisheni ya Ulaya imesema itatoa mapendekezo yake ikiwa Ankara itashindwa kufanya marekebisho juu kulinda uhuru wa kujieleza na kushindwakufikia muwafaka na Cyprus hadi katikati ya mwezi December.

Nae Rais wa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Jose Manuel Baroroso akitilia mkazo jitihada za kidiplomasia kutumika juu ya Uturuki dhidi ya masharti iliyowekewa, alisema.

“Hivi sasa tunategemea maneno yatatuongoza katika vitendo haraka iwezekanavyo“

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com