1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BRUSSELS:mzozo wa Iran bado waendelea

Azimio jipya la Umoja wa ulaya linalopendekeza kuiwekea vikwazo Iran juu ya mpango wake wa Kinuklia linapunguza orodha ya bidhaa ambazo Iran haiwezi kununua au kuuza na badala yake kuruhusu Urusi kujenga na kutia mafuta kinu cha kinuklia inachokijenga Iran.

Uingereza Ufaransa na Ujerumani zimepeleka masharti hayo mbele ya baraza la usalama la Umoja wa mataifa hapo jana ijumaa na zinatarajia baraza hilo litapiga kura kabla ya Krismasi kuhusu hatua hiyo.

Lakini haijabainika ikiwa Urussi ambayo inakura ya turufu kwenye baraza hilo itaunga mkono,itakaa au haitopiga kura juu ya hatua hiyo.

Vikwazo hivyo vilivyopendekezwa vinatokana na Iran kukaidi tarehe ya mwisho ya Agosti 31 iliyowekwa na Umoja wa mataifa kwamba ikomeshe mpango wake wa kinuklia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com