1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels. Wanadiplomasia wa umoja wa Ulaya watimuliwa Ethiopia.

20 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD0r

Wanadiplomasia wawili wa umoja wa Ulaya waliokamatwa nchini Ethiopia kwa madai ya kujaribu kuwatorosha wahalifu kwenda Kenya wamefukuzwa nchini humo.

Afisa wa umoja wa Ulaya amethibitisha leo kuwa watu hao waliondolewa kwa ndege kwenda Kenya usiku wa jana , lakini amekataa kuwataja wanadiplomasia hao ama kutaja uraia wao.

Televisheni ya taifa , ikiwakariri maafisa wa Ethiopia, imesema kuwa watu hao wawili walikamatwa kusini mwa Ethiopia karibu na mji wa mpakani wa Moyale wakiwa na idadi ambayo haikutajwa ya wahalifu ambao wanatafutwa na maafisa hao wamezuiwa kabisa kuingia tena nchini humo.

Umoja wa Ulaya ni moja kati ya wafadhili wakubwa wa Ethiopia lakini umekuwa ukiikosoa sana serikali ya nchi hiyo kwa kuwakamata viongozi wa upinzani na waandishi wa habari tangu ghasi kuikumba nchi hiyo baada ya mvutano kuhusu matokeo ya uchaguzi mwaka jana.