BRUSSELS: Urusi isilete mtengano katika Umoja wa Ulaya
19 Mei 2007Matangazo
Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barroso,ameionya Urusi dhidi ya kuleta mtengano katika umoja huo.Amesema,maslahi za nchi za Ulaya ya Mashariki zilizo wanachama wa Umoja wa Ulaya ni halali,sawa sawa na maslahi za nchi za Ulaya ya Magharibi.