1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels. Umoja wa Ulaya wafanikiwa kupata muafaka.

24 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBos

Viongozi wa umoja wa Ulaya wamefikia makubaliano ya mfumo wa mkataba mpya wa mageuzi.

Baada ya mazungumzo ya usiku kucha mjini Brussels, kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema kuwa kundi la mataifa hayo ya Ulaya limefikia muafaka mzuri juu ya mfumo wa upigaji kura, ambao utaendelea hadi mwaka 2017.

Poland ilitishia kuzuwia makubaliano hayo.

Mataifa hayo 27 wanachama yamekubaliana kujadiliana kuhusu mkataba huo wa mageuzi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu, na baada ya hapo kuuidhinisha ifikapo katikati ya mwaka 2009.

Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair, ambaye nchi yake iliukataa muswada uliopita wa makubaliano, amesema kuwa nchi yake imeweza kupata maridhiano muhimu.

Rais wa halmashauri ya umoja wa Ulaya Jose Manuel Barosso ameliambia gazeti la kila Jumapili nchini Ujerumani la Bild am Sonntag kuwa makubaliano hayo ya mkataba yanaondoa shaka juu ya uwezo wa umoja wa Ulaya kuchukua hatua.