BRUSSELS: Mwito kwa Waisraeli na Wapalestina kukomesha mapambano | Habari za Ulimwengu | DW | 05.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BRUSSELS: Mwito kwa Waisraeli na Wapalestina kukomesha mapambano

Umoja wa Ulaya umesema unasikitishwa na hasara ya maisha ya raia wasio na hatia katika Ukanda wa Gaza na umewahimiza Waisraeli na Wapalestina kukomesha mapambano.Zaidi ya watu 40 wameuawa katika mashambulio ya siku nne yaliofanywa na vikosi vya Israel ndani na ukingoni mwa mji wa Beit Hanoun katika Ukanda wa Gaza.Rais Mahmoud Abbas wa Wapalestina,ametoa mwito kwa Umoja wa Mataifa kuingilia kati kuzuia mashambulio ya Israel.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com