1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Mkataba mpya wa Umoja wa Ulaya wakubaliwa

23 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBp9

Viongozi wa Umoja wa Ulaya katika mkutano wa kilele wa umoja huo mjini Brussels,Ubeligiji wamekubaliana kuanzisha majadiliano ya mkataba mpya.

Makubaliano hayo yalipatikana baada ya Poland kukubali pendekezo la maafikiano kuhusu haki za kupiga kura katika Umoja wa Ulaya.

Kuambatana na pendekezo hilo jipya,utaratibu wa kupiga kura wa hivi sasa utaendelea kutumika hadi mwaka 2017.Uingereza pia imeridhiwa katika masuala muhimu,ikiwa ni pamoja na kubakia na mamlaka ya kitaifa kuhusu masuala ya haki na polisi na vile vile mkataba wa Umoja wa Ulaya hautoingilia sheria za Uingereza.Wakati huo huo, rais wa Ufaransa,Nicolas Sarkozy amesema,mkataba mpya wa Umoja wa Ulaya utahifadhi haki za wafanyakazi,utapinga ushindani mkali na uchumi wa soko huru kama ule wa Marekani.