1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya waanza mazungumzo

23 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBg0

Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wameanza mazungumzo yanayolenga kukamilisha katiba ya nchi 27 wanachama wa umoja huo.

Waziri mkuu wa Portugal Luis Amado ambae nchi yake ndio mwenyekiti wa Umoja wa Ulaya kwa sasa amesema kuwa mawaziri hao wanataka kukamilisha mpango huo kabla ya mkutano wa kilele wa viongozi wa nchi za Umoja wa Ulaya unaopangiwa kufanyika mwezi Oktoba.

Poland imehoji tena juu ya katiba hiyo ya Umoja wa Ulaya ijapokuwa waziri wake wa mambo ya nje bibi Anna Fotyga amesema kuwa nchi yake haipingi mswaada wa katiba hiyo.

Wakati huo huo kamisheni ya umoja wa ulaya imetoa kiasi cha Euro milioni tano msaada wa kibinadamu kuzisadia jamii za kaskazini mwa Kenya ambazo zimeathiriwa vibaya na ukame hali ngumu ya maisha na pia zinakabiliwa na matatizo ya lishe bora.

Msaada huo ni ongezeko katika msaada wa Euro milioni nne zilizotolewa mwaka huu pamoja na msaada mwingine unaotolewa na kamisheni hiyo ya umoja wa ulaya kwa matayarisho ya athari za ukame katika upembe wa Afrika Kenya ikiwa ni miongoni mwa nchi hizo. Kamishna wa maendeleo na misaada ya kiutu wa umoja wa ulaya Louis Michel amesema kamisheni ya umoja wa ulaya inatoa misaada ili kuzuia mzozo wa kibinadamu katika eneo la kaskazini mwa Kenya.