Brussels. Mawaziri kukutana na wenzao wa umoja wa Ulaya. | Habari za Ulimwengu | DW | 11.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Brussels. Mawaziri kukutana na wenzao wa umoja wa Ulaya.

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa umoja wa Ulaya watakutana na mawaziri wenzao wa umoja wa mataifa ya Kiarabu , Arab League , siku ya Jumatatu ili kuimarisha juhudi za kuleta amani za mataifa ya Kiarabu yenye lengo la kutanzua mzozo kati ya Israel na Palestina.

Marekani na Israel zimeonyesha shauku katika mpango huo wa amani ambao unatoa kwa Israel uhusiano wa kawaida na mataifa yote ya Kiarabu kwa kupata kutoka Israel kuyaondoa majeshi yake hadi katika mipaka ya 1967 na kuundwa kwa taifa la Palestina.

Mpango huo wa amani wa mataifa ya Kiarabu umekuwa umetupwa kando tangu 2002 baada ya kukataliwa mara kwa mara na Israel, lakini ulifufuliwa katika mkutano wa mataifa ya Kiarabu mjini Riyadh mwezi wa March.

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa Misr na Jordan , wakiwa kama kundi la kushughulikia suala hilo la umoja wa mataifa ya Kiarabu , wamemweleza waziri wa mambo ya kigeni wa Israel Tzipi Livni, ukiwa ni mkutano wa kwanza wa aina hiyo tangu kuundwa kwa taifa la Kiyahudi mwaka 1948.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com