1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BRUSSELS: Hatima ya Kosovo kuamuliwa na Umoja wa Mataifa

Wajumbe wa Umoja wa Ulaya na Rais Boris Tadic wa Serbia wanajaribu kuafikiana kuhusu mgogoro wa jimbo la Kosovo.Hatima ya jimbo hilo ambalo tangu mwaka 1999 huongozwa na Umoja wa Mataifa, itaamuliwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.Wakati ambapo Marekani inataka jimbo hilo lipewe uhuru wa kujiongoza upesi iwezekanavyo, Urusi imetishia kutumia kura ya turufu kupinga uamuzi wa aina hiyo.Moscow imesema,itakubali tu suluhisho ambalo litaidhinishwa na Serbia.Wakati huo huo Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya,Jose Manuel Barroso ametoa wito kwa serikali ya Serbia ishirikiane kwa dhati na isaidie kutenzua mgogoro wa Kosovo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com