1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRASILIA:Mpambe wa Lula Da Silva ashtakiwa kwa kuhusika na Rushwa

28 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBVG

Mahakama kuu ya Brazil imemshtaki rasmi aliyekuwa mpambe wa ngazi ya juu war ais Luiz Inacio Lula da Silva kufuatia madai ya kuhusika katika kashfa ya rushwa ya kisiasa.

Jose Dirceu anadaiwa kuhusika katika kuendesha kashfa ya mlungula ambayo pia iliwatia mashakani na kusababisha kujiuzulu kwa mawaziri kadhaa mwaka 2005 pamoja na maafisa wengine wa chama cha PT cha rais Da Silva.

Kwa mujibu wa mwanasheria mkuu Fernando de Souza mwaka 2006 Jose Dirceu alihusika katika ufujaji wa fedha,kukwepa kulipa kodi,ufisadi pamoja na kuwa mbadhirifu wa mali ya serikali.

Mahakama hiyo pia hapo jan iliwashtaki rasmi viongozi wengine wa vyama vingine vya kisiasa vinavyoshirikiana na chama tawala cha PT.

Kashfa hiyo inasemekana ililengwa kusaidia katika kampeini ya kukibakisha chama cha PT madarakani.