1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BLANTYRE:Wafungwa 495 waachiwa huru na Rais Mutharika

12 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBja

Rais wa Malawi Bingu wa Mutharika ameidhinisha kuachiwa huru mapema kwa wafungwa 495 ikiwa ni sehemu ya kusherehekea miaka 43 ya uhuru nchini humo.

Idadi hiyo ji asilimia 4 ya wafungwa wote ambao ni zaidi ya alfu 10 nchini Malawi katika jela zote 23.Kulingana na msemaji wa Magereza nchini humo Tobias Nowa hatua hiyo inatoa afueni katika matumizi ya jela kwani zimejaa pomoni.

Rais Mutharika aliyeingia madarakani mwaka 2004 kwa kawaida huidhinisha kuachiwa kwa wafungwa wanaozuiliwa kwa makosa madogo wakati wa sherehe za kuadhimisha uhuru wa nchi ,Krismasi na Pasaka.