1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Bingwa wa kombe la mataifa ya Afrika kupatikana leo

Ni Mapharao au Cameroon?

MICHEZO -ACCRA

Leo ni leo katika uwanja wa michezo wa Ohene Djan nchini Ghana ambapo mabingwa Misri watapambana na Cameroon katika finali ya kuwania kombe la mataifa ya Africa.Nahodha wa timu ya Cameroon Rigobert Song amesema timu yake imekuwa ikifanya makosa mengi uwanjani lakini hilo limesharekebishwa na hivyo leo wanaweka matumaini ya kukitwaa kikombe.Mapharao Misri wanatazamiwa kuwa ngangari uwanjani ikiwa mshambuliaji wao Mohammed Zidan atakuwa fit kutokana na jeraha la goti.Jana wenyeji Ghana walichukua nafasi ya tatu baada ya kuwalaza codivoier mabao 4 kwa 2.

Mchezo wa leo utaangaliwa na viongozi mbali mbali akiwemo waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeir ambaye yuko ziarani katika eneo hilo.

 • Tarehe 10.02.2008
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/D591
 • Tarehe 10.02.2008
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/D591

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com