BERLIN:Umoja wa Ulaya una wasiwasi juu ya hali ya kisiasa Ukraine | Habari za Ulimwengu | DW | 28.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN:Umoja wa Ulaya una wasiwasi juu ya hali ya kisiasa Ukraine

Umoja wa ulaya umezungumzia wasiwasi wake juu ya hali ya kisiasa nchini Ukraine.

Mwenyekiti wa Umoja huo Ujerumani imetoa taarifa kwamba kuna wasiwasi uliojitokeza ambapo upande wa upinzani Ukraine haufanyi juhudi za kutosha za kufimkia muafaka juu ya mzozo wa Kisiasa.

Taarifa ya Umoja wa Ulaya imekuja baada ya waandamanaji 60 elfu kuingia majiani katika mji mkuu Kiev kupinga uamuzi wa karibuni wa rais Viktor Yushenko wa kulivunja bunge na kuitisha uchaguzi wa mapema.

Waziri mkuu anayeegem,ea upande wa Urussi Viktor Yanukovich amelitolea mwito bunge kupuuza amri ya rais akisema bwana Yushenko hana uwezo kikatiba kulivunja bunge.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com