1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Merkel akutana na Dalai Lama pamoja na pingamizi la China

24 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBNA

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amekuwa na mazungumzo maalum na kiongozi wa kidini wa Tibet, Dalai Lama.

Kansela Merkel amefanya mazungumzo hayo pamoja na kuwepo kwa lawama kutoka China za kumtaka kutokutana na kiongozi huyo.

Katika kuonesha kutoridhishwa kwake na hatua hiyo ya Kansela Merkel, China ilijiondoa katika ushiriki wake kwenye mkutano wa masuala ya sheria kati ya nchi mbili hizo mjini Munich.

Wiki iliyopita, serikali ya China ilimuita balozi wa Ujerumani mjini Beijing kulalamika ya juu ya hatua ya Ujerumani kuingilia mambo ya ndani ya China.

Ujerumani kwa upande wake imesema kuwa inataka kuendelea kuwa na uhusiano mzuri na China na kwamba inaunga mkono nia ya watu wa Tibet kutaka kujitawala lakini si kuwa taifa huru.

China inaitawala Tibeti toka mwaka 1951 na kiongozi huyo wa kidini Dalai Lama amekuwa akiishi uhamishoni nchini India toka mwaka 1959.