BERLIN:Jeshi la Ujerumani kutoa msaada wa kitalaamu zaidi likihitajika | Habari za Ulimwengu | DW | 12.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN:Jeshi la Ujerumani kutoa msaada wa kitalaamu zaidi likihitajika

Waziri wa maendeleo wa Ujerumani bibi Heidemarie Wieczorek-Zeul amesema kwamba uwezekano upo wa Ujerumani kutoa mchango zaidi katika harakati za kulinda amani katika jimbo la Darfur nchini Sudan.

Kwa sasa Ujerumani inashughulikia maswala ya kilojistiki ya usimamizi na mikakati ya usafirishaji kwa ndege katika jimbo la Darfur nchini Sudan.

Jeshi la Ujerumani Bundeswehr lina mamlaka ya kubakia katika jimbo la Darfur hadi katikati ya mwezi Desemba na linaweza kutoa mchango wa wataalamu wake wa kijeshi hadi kufikia mia 200 katika kukisaidia kikosi cha umoja wa Afrika huko magharibi mwa Sudan.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com