1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Dalai Lama aalikwa na Kansela wa Ujerumani,China yalalamika

15 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBPZ


Wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani imearifu kwamba balozi wa Ujerumani nchini China aliitwa na serikali ya nchi hiyo kujadili uamuzi wa Kansela wa Ujerumani bibi Angela kukutana na kiongozi wa dini Dalai Lama.

Kansela Merkel anatarajia kukutana na kiongozi huyo wa kidini kwenye ofisi yake mjini Berlin wiki ijayo.

Dalai Lama ni kiongozi wa kidini anaeongoza harakati za kupigania uhuru wa jimbo la Tibet ambalo lipo chini ya utawala wa China.