1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN.Baraza la mawaziri lapitisha uamuzi wa kupeleka ndege za upelelezi Afghanistan

7 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCUE

Baraza la mawaziri la Ujerumani limepitisha uamuzi juu ya kupeleka ndege sita za upelelezi aina ya Tornado nchini Afghanistan.

Uamuzi huo hata hivyo lazima upitishwe na bunge la Ujerumani linalotarajiwa kuupigia kura mwezi Machi.

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Franz Josef Jung amesema….

O ton…… Ukweli ni kwamba wapiganaji wa taliban wanajitayarisha kuzidisha mashambulio, takriban magaidi 2000 wako tayari kujitoa muhanga na kwa maoni yangu nafikiria ni lazima tuhakikishe kwamba hatua madhubuti za usalama wa raia zinachukuliwa.

Waziri Jung amelitaka bunge la Ujerumani kuidhinisha uamuzi wa kupelekwa ndege hizo za upelelezi nchini Afghanistan.

Iwapo hatua hiyo itaidhinishwa na bunge ndege hizo aina ya Tornado zitapelekwa nchini Afghanistan katikati ya mwezi Aprili.

Zoezi hilo la miezi sita litaigharimu Ujerumani kiasi cha Euro milioni 35.

Ujerumani ina askari 2,700 katika eneo la kaskazini mwa Afghanistan ikiwa ni sehemu ya jeshi la kimataifa linaloongozwa na NATO katika kulinda amani nchini Afghanistan.