BERLIN: Ujerumani yatoa msaada zaidi wa fedha kwa Somalia | Habari za Ulimwengu | DW | 23.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN: Ujerumani yatoa msaada zaidi wa fedha kwa Somalia

Wizara ya mashauri ya kigeni ya Ujerumani imetenga fedha zaidi kiasi cha euro milioni 1.4 kugharamia misaada ya kiutu nchini Somalia. Tangu machafuko yalipozuka nchini Somalia mwezi Disemba mwaka jana euro milioni 1.65 zimetumika kwa misaada nchini humo.

Milioni moja itapewa kamati ya kimatafia ya shirika la msalaba mwekundu kuwasaidia waathiriwa wa mafuriko na mapigano. Zaidi ya euro laki mbili zitapewa shirika la misaada la kimataifa la CARE tawi la Ujerumani.

Miradi zaidi ya kuwasaidia wasomali imeandaliwa pia na mashirika yasiyo ya kiserikali ya hapa Ujerumani.

Kuzuka kwa mapigano mwishoni mwa mwaka jana nchini Somalia kulisababisha hali ya kibinadamu kuwa mbaya na kuyafanya mashirika ya misaada ya kigeni ambayo yana wafanyakazi wachache nchini humo, kutoweza kutoa huduma zao.

Mwaka jana wizara ya kigeni ya Ujerumani ilitoa takriban euro milioni 2.47 kwa ajili ya Somalia. Kati ya kiwango hicho, milioni 1.52 zitatumika ndani ya Somalia huku nyengine euro elfu 950 zikiwa zimetengwa kuwahudumia wakimbizi wa kisomali nchini Kenya.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com