1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Berlin. Ujerumani yaishutumu Burma.

Ujerumani imeshutumu kukamatwa kwa wapinzani wa utawala wa kijeshi nchini Burma . Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni mjini Berlin amesema kuwa hatua hizo zilizochukuliwa na utawala huo wa kijeshi zitaleta athari kubwa .Amesema kuwa baraza la usalama la umoja wa mataifa na mawaziri wa mambo ya kigeni wa umoja wa Ulaya wanaokutana baadaye wiki hii wataangalia uwezekano wa kuwekea vikwazo maalum kwa viongozi wa kijeshi Burma. Ujerumani pia imejiunga na nchi nyingine katika madai ya kuachiliwa kwa wafungwa wote wa kisiasa, ikiwa ni pamoja na kiongozi wa upinzani Aung San Suu Kyi. Wakati huo huo , utawala wa kijeshi wa Burma umemteua afisa atakaye imarisha uhusiano na mshindi wa nishani ya amani ya Nobel. Wazo hilo lilitolewa na mjumbe maalum wa umoja wa mataifa Ibrahim Gambari wakati wa ziara yake nchini Burma wiki iliyopita. Msemaji wa shirika la kutoa misaada la msalaba mwekundu Carla Haddad ameikosoa serikali ya Myanmar kwa kushindwa kuwapa nafasi kuwaona watu walioko kizuizini.

Wakati huo huo China imesema leo kuwa inapinga mbinyo wa aina yoyote mkubwa dhidi ya nchi mshirika wake wa karibu Myanmar kutokana na ukandamizaji wa nguvu wa maandamano wa kidemokrasia, ikionya kuwa hali hiyo inaweza kuongeza hali ya wasi wasi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com