BERLIN : Ujerumani yaahirisha kutuma ndege Afghanistan | Habari za Ulimwengu | DW | 13.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN : Ujerumani yaahirisha kutuma ndege Afghanistan

Serikali ya Ujerumani imesema itaahirisha uamuzi wa kupeleka ndege za upepelezi aina ya tornado kusini mwa Afghanistan hadi baada ya mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Kujihami wa Mataifa ya Magharibi NATO utakaofanyika katika kipindi cha wiki mbili zijazo.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeir amefuta matamshi yaliotolewa awali kutoka kwa msemaji wa chama cha SPD bungeni Peter Struck kwamba ndege hizo sita zitapelekwa kusadia vikosi vya NATO.Haiko dhahiri iwapo mamlaka ya Ujerumani itajihusisha na kutanuliwa kwa operesheni za NATO kwenye eneo tete la kusini mwa Afghanistan.

Wakati huo huo polisi ya Afghanistan imesema kwamba shambulio la anga la NATO kwenye maficho ya waasi kusini mwa nchi hiyo limeuwa zaidi ya watuhumiwa 16 wa kundi la Taliban na raia 13 hapo Alhamisi katika wilaya ya Garamsir ya jimbo la vurugu la Helmand.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com