1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Ujerumani yaadhimisha miaka 16 ya muungano

3 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD6j

Ujerumani leo inaadhimisha miaka 16 tangu eneo la mashariki lilipoungana na eneo la magharibi. Maelfu ya wajerumani wanatarajiwa kujitokeza mjini Kiel kwa sherehe zitakazohudhuriwa na rais Horst Köhler na kansela Angela Merkel.

Wakati huo huo, waziri wa uchukuzi na maendeleo ya miji, Wolfganda Tiefensee, amesema ingawa ufanisi mkubwa umepatikana katika miaka 16 iliyopita, maeneo ya mashariki yaliyozorota kiuchumi, yataendelea kulitegemea eneo la magharibi kwa miaka 15 hadi 20 ijayo.