1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Ujerumani kutobadili mamlaka yake Afghanistan

14 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBPx

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeir amesema Ujerumani haina mpango wa kubadili mamlaka ya shughuli zake za kulinda amani nchini Afghanistan ambayo inawafunga wanajeshi wake kuweko kwenye eneo lenye utulivu fulani kaskazini mwa nchi hiyo.

Steinmeir anasema watatilia mkazo kuwepo kwa wanajeshi wao katika eneo la kaskazini na kwa upande wa majukumu wataelekeza njia ya kulipa mafunzo jeshi la Afghanistan.

Kauli ya Steinmeir inakuja kufuatia mkutano wake na Katibu Mkuu wa Umoja wa Kujihami wa Mataifa ya Magharibi NATO Jaap de Hoop Scheffer mjini Berlin.Marekani na nchi nyengine wanachama wa NATO zimekuwa zikiihimiza Ujerumani kuachana na vikwazo nyenye kuzuwiya wanajeshi wa Ujerumani kusaidia kupamabana na kuibuka upya kwa wanamgambo wa Taliban.

Wakati Scheffer akikanusha kwamba NATO imekuwa ikiishinikiza Ujerumani kutuma vikosi vyake kwenye maeneo ya vurugu kusini mwa Afghanistan amekiri kwamba makamanda wa NATO wangelipendelea kutokuwepo na vikwazo juu ya suala la uwekaji wa vikosi.