1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin: Uchumi wa Ujerumani waboreka 2006

22 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCPm

Uchumi wa Ujerumani uliimarika mwaka uliopita 2006. Kwa mujibu wa ripoti iliotolewa na ofisi kuu ya masuala ya takwimu ni mara ya kwanza Ujerumani taifa kubwa la kiuchumi barani Ulaya iliweza kufikia kiwango cha kutovuka nakisi ya bajeti ya 3 asili mia uliowekwa kwa nchi wanachama wa umoja wa ulaya, huku bajeti yake ikifikia nakisi ya 1.7 asili mia, ikiwa ni mara ya kwanza katika muda wa miaka 5. Uchumi kwa jumla ulikua mwaka jana kwa nukta tisa asili mia, na kufikia kiwango cvha ongezeko la 2.7 asili mia.