1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Berlin. Uchumi wa Ujerumani kuongezeka mwakani.

Waziri wa uchumi wa Ujerumani Michael Glos amesema anatarajia ukuaji zaidi wa uchumi katika mwaka 2007 kuliko hapo kabla ilivyofikiriwa.

Glos ameueleza hali ya uchumi nchini Ujerumani kuwa ni bora kuliko wakati mwingine wowote tangu mataifa mawili ya Ujerumani kuungana na amesema kuwa anafikiri hali hiyo italeta hali bora katika soko la kazi la nchi hiyo katika mwaka ujao.

Ujerumani imekuwa ikitarajia ukuaji wa asilimia 1.4 katika mwaka 2007.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com