1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Rais wa Chile anahimiza vitega uchumi kutoka Ujerumani

20 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD13

Ujerumani na Chile zinataka kuimarisha zaidi ushirikiano wao.Baada ya kukutana na rais Michelle Bachelet wa Chile mjini Berlin,Kansela Angela Merkel wa Ujerumani itaisaidia mageuzi ya kisheria yanayofanywa katika nchi hiyo ya Amerika ya Kusini.Wakati wa ziara yake nchini Ujerumani, rais Bechelet alie msoshalisti anataka kuyahimiza makampuni ya Kijerumani kuweka vitega uchumi nchini mwake na hivyo kuwapatia wananchi wa Chile nafasi za kazi.Ujerumani katika Umoja wa Ulaya,ni mshirika muhimu kabisa wa Chile katika sekta ya biashara.