BERLIN : Merkel kukutana na Olmert | Habari za Ulimwengu | DW | 12.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN : Merkel kukutana na Olmert

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani na Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert wanatazamiwa kuwa na mazungumzo mjini Berlin leo hii.

Olmert anatarajiwa kuzungumzia mahsusi mzozo wa nuklea na Iran unaondelea kurindima pamoja na ziara ya hivi karibuni nchini Syria iliofanywa na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Seinmeir.Waziri Mkuu huyo wa Israel aliikosowa vikali ziara hiyo.

Hapo jana Olmert alizusha taharuki huko nyumbani kwa kumaanisha wakati wa mahojiani na radio ya Ujerumani kwamba nchi yake inamiliki silaha za nuklea.Wanasiasa wa upinzani nchini Israel wametowa wito wa kujiuzulu kwake lakini maafisa wa serikali walikanusha kwa haraka kwamba alikuwa amemaanisha kuwa Israel inayo au ilikuwa ikitaka kumiliki silaha za nuklea.

Huko nyuma Israel imekuwa haioku wazi juu ya uwezekano wa kumiliki silaha hizo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com