1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin marathon na Gebreselassie

Ramadhan Ali28 Septemba 2007

Macho ya wanariadha yakodolewa jumapili hii Berlin ambako muethiopia Gebreselassie analenga kuivunja rekodi ya mkenya Paul Tergat.

https://p.dw.com/p/CHax
Ujerumani na Brazil finali
Ujerumani na Brazil finali

Bundesliga-Ligi ya Ujerumani, yarudi nayo uwanjani huku Bayer Leverküsen inayonyatia kutoka nafasi ya pili ya ngazi ya Ligi, ikitumai kuitundua Bayern Munich leo kutoka kileleni.

Macho ya wanariadha yatakodolewa kesho mjini Berlin kwa mbio za Berlin-marathon wakati mjini Nairob,Kenya , leo ni zamu tena ya mashindano ya riadha ya Tusker yakiingiza bingwa wa mita 800 kutoka Afrika Kusini Mbulaeni Mulaudzi na bingwa wa dunia wa Kenya Janeth Jepkosgei.

Timu za wasichana za Ujerumani na Brazil, zinakumbana kesho kwa mara ya kwanza katika finali ya kombe la dunia.

Ujerumani ndio mabingwa watetezi na walikwishatoa salamu na mapema kwa Brazil pale katika mpambano wao wa kwanza wa kombe hili la dunia walipojaza kikapu cha jirani zao Brazil-Argentina –mabao 11:0.

Ujerumani kesho lakini,haitadiriki kutia tena mabao mengi kama hayo,kwani wasichana wa Brazil walioitoa Marekani kwa mabao 3:0 kukata tiketi ya finali ya kesho hawatawaachia.Hata bao 1 litatosha ikiwa warejee na kombe Ujerumani.

Watabidi kumchunga Mata,mshambulizi hatari wa Brazil aliekomea tayari mabao si chini ya 5 .

Ujerumani iliitoa Norway,mahasimu wao wakubwa wakiwa njiani kwa finali ya kesho.Ushindi kwa ni muhimu,kwani Ujerumani inapanga kugombea kuandaa kombe lijalo la dunia la wanawake mwa 2011.

Kwa mashabiki wa Bundesliga,hawahitaji kungoja hadi kesho jumapili:Bayer Leverkusen ,inavizia tu Bayern Munich inayoongoza Ligi wakati huu, iteleze katika changamoto yao ya leo ili waparamie kileleni mwaBundesliga.

Kati ya wiki ,Bayern Munich ilivuma kwa kishindo ilipoirarua Cottbus kwa mabao 5-0-shukurani kwa mabao 3 pekee ya Miroslav Klose.

Leverkusen itakuwa nyumbani.Werder Bremen wanaumana na Armenia Bielefeld wakati Bochum inacheza na Nüremberg.

Hamburg inacheza na jirani zao Wolfsburg ikiwachia B.Dortmund kunyan’ganyia pointi 3 na Karsruhe.Hansa Rostock ina wakaribisha nyumbani mabingwa Stuttgart ambao wakati huu wako hoi.

Kesho changamoto 2 zitakamilisha duru hii ya Bundesliga:Hannover na Duisburg wakati Energie Cottbus itabidi ifute mabao 5 ya majuzi kwa kutamba mbele ya Frankfurt.

Katika Premier League-ligi ya uingereza,Arsenal inayotapia ubingwa ina mtihani mgumu leo mbele ya west Ham na hata kocha wao Arsene Wenger anaungama.

Mlolongo wa kutoshindwa mechi 10 katika mashindano mbali mbali,umeipa Arsenal nafuu mbele ya mabingwa Manchester United,makamo-bingwa Chelsea na hata Liverpool.

Manchester Utd. ina miadi na Birmingham wakati Chelsea ni wenyeji wa Fulham.Waigan Athletic inacheza na Liverpool.

Katika La Liga-ligi ya Spain,Real Madrid ilirudi juzi alhamisi kileleni baada ya kuitimua Real betis 2-0.

Kesho, wanariadha kutoka kila pembe ya dunia watakuwa barabarani mjini Berlin kwa mbio za mwaka huu za Berlin marathon.Usoni kabisa atakuwa Haile Gebreselassie wa Ethiopia ambae analenga kuifuta rekodi ya dunia ya mkenya Paul Tergat alieiweka huko huko Berlin.Mabingwa wengine wa marathon kutoka Kenya na Ethiopia watapeana changamoto.

Huko Nairobi,Kenya,itakua zamu leo ya mbio za riadha za Tusker:Ni mastadi 2 tu mashuhuri waliojitolea kuingia uwanjani na wote wa mita 800 wanaume na wanawake:

Upande wa wanaume, ni bingwa wa Afrika kusini ,mshindi wa medali ya fedha wa olimpik Mbulaeni Mulaudzi, na kutoka Kenya atatamba bingwa wa dunia Janeth Jepkosgei.

Muladudzi ndie aliekimbia muda mbora msimu huu lakini hatapambana na bingwa wa dunia wa Kenya Alfred Kirwa Yego.Mashindano haya ya leo yanafanyika katika Uwanja wa taifa wa Nyayo.