BERLIN: Maandamano kupigwa marufuku karibu na mkutano | Habari za Ulimwengu | DW | 16.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN: Maandamano kupigwa marufuku karibu na mkutano

Maafisa nchini Ujerumani wamesema,waandamanaji hawatoruhusiwa kukaribia eneo ambako mwezi ujao kutafanywa mkutano wa kilele wa mataifa tajiri yaliyoendelea kiviwanda G-8.Kwa mujibu wa polisi, kuanzia tarehe 5 Juni,ikiwa ni siku moja kabla ya mkutano huo wa kilele,waandamanaji watapigwa marufuku eneo la kilomita tano linalozunguka jengo la mkutano mjini Heiligendamm.Wakati wote wa mkutano huo,maandamano yatapigwa marufuku pia kwenye uwanja wa ndege wa Rostock unaotumiwa na mji wa Heiligendamm.Ujerumani inataraji hadi wanaharakati 100,000 wanaopinga utandawazi, kufanya maandamano dhidi ya viongozi wa nchi nane tajiri zilizoendelea kiviwanda duniani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com