1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Ehud Olmert ziarani nchini Ujerumani

12 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCk6

Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel leo anakutana na waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert aliewasili Berlin kwa ziara yake ya kwanza nchini Ujerumani. Mgogoro kati ya Waisraeli na Wapalestina,matokeo ya nchini Lebanon na ugomvi unaohusika na mradi wa nyuklia wa Iran ni masuala yatakayopewa umuhimu wakati wa mazungumzo yao.Suala la mabishano linahusika na Syria.Olmert,alikosoa ziara iliyofanywa hivi karibuni na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier nchini Syria.Olmert,baada ya ziara ya Berlin ataelekea Rome ambako atakutana na waziri mkuu wa Italia Romano Prodi.