1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT:Maandamano makuu yameitishwa na Hezbollah siku ya Ijumaa

30 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCny

Nchini Lebanon,chama cha Hezbollah kimeitisha maandamano makuu mjini Beirut siku ya Ijumaa. Chama cha upinzani cha Lebanon ambacho huelewana na Syria kinataka kuiangusha serikali ya waziri mkuu Fouad Siniora iliyo dhidi ya Syria.Serikali ya Siniora yenye uwingi mkubwa bungeni inaungwa mkono na nchi za Magharibi.Lebanon imegawika kati ya wale wanaoiunga mkono Syria na wale wanaoipinga,hasa tangu kuuawa kwa waziri mkuu wa zamani Rafik Hariri pamoja na mauaji mengine ikiwa ni pamoja na kuuliwa kwa waziri wa viwanda Pierre Gemayel katika mwezi huu.Serikali inayoipinga Syria inailaumu nchi hiyo na mawakala wake nchini Lebanon kuhusika na mauaji hayo.Vile vile Syria inatuhumiwa kuwa inajaribu kuzuia kuundwa kwa mahakama ya kimataifa kusikiliza kesi dhidi ya wale wanaoshukiwa kuhusika na kifo cha Hariri.