1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT : Watu 3 wauwawa katika ghasia na 130 wajeruhiwa

24 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCYL

Wafuasi wa upinzani wameondoka kwenye barabara za mji mkuu wa Beirut walizokuwa wameziwekea vizuizi baada ya watu watatu kuuwawa katika maandamano ya upinzani yalioongozwa na kundi la Hezbollah.

Waziri Mkuu wa Lebanon Fouad Siniora ameapa kusimama kidete dhidi ya kile alichokiita kuwa vitisho wakati wa mgomo huo wa taifa.Polisi imesema watu watatu wameuwawa katika mji wa Tripoli na miji miwili ya katikati ya Lebanon hapo jana wakati wa mapambano kati ya wafuasi wa serikali na waandamanaji wa upinzani na zaidi ya watu 130 wamejeruhiwa.

Siniora anayeungwa mkono na Marekani ametowa wito kupitia televisheni kufanyika kwa kikao cha bunge cha dharura kuzima mgogoro huo.Maandamano hayo yanakwenda sambamba na mkutano wa wafadhili mjini Paris Ufaransa kusaidia kuugharimia uchumi wa Lebanon ulioelemewa na madeni.

Ujerumani ambaye ni Rais wa Umoja wa Ulaya umezitaka pande zote nchini Lebanon kuingia kwenye mazungumzo kuutatuwa mgogoro huo na kujiepuesha na umwagaji damu.