1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Washukiwa sita wa njama ya kuziripua treni za abiria washtakiwa

12 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCbU
Javier Solana
Javier SolanaPicha: AP

Jaji wa mahakama ya mjini Beirut amewasilisha mashtaka dhidi ya raia sita wa Lebanon kuhusiana na majaribio ya kuzilipua treni mbili za abiria nchini Ujerumani mwaka jana.

Jaji huyo amependekeza washukiwa wote wahukumiwe kifungo cha maisha gerezani. Washukiwa watano wanazuiliwa na polisi wa Lebanon.

Kesi ya mshukiwa mmoja anayezuiliwa na polisi hapa Ujerumani itasikilizwa bila yeye kuwepo. Kwa mujibu wa sheria ya Lebanon, mshukiwa hawezi kuwasilishwa kwa Ujerumani ili ashtakiwe.

Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka ya kutega mabomu kwenye treni za abiria katika mkoa wa North Rhine Westphalia mwezi Julai mwaka jana. Mabomu yote mawili yalikuwa na hitilafu na yakashindwa kulipuka.