BEIRUT: Vitendo vya uadui havitostahmiliwa na Israel | Habari za Ulimwengu | DW | 08.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BEIRUT: Vitendo vya uadui havitostahmiliwa na Israel

Waziri Mkuu wa Lebanon Fouad Siniora ameituhumu Israel kuwa imevuka mpaka wa Lebanon.Siniora ametamka hayo baada ya buldoza la Waisraeli kuvuka mpaka uliowekwa na Umoja wa Mataifa.Vikosi vya Kiisraeli vilikuwa vikisaka mabomu yaliozikwa na wanamgambo wa Hezbollah.Kwa sababu ya tukio hilo,vikosi vya Lebanon vilifyatua risasi dhidi ya buldoza na wanajeshi wa Kiisraeli pia walijibu kwa risasi.Hakuna aliejeruhiwa katika tukio hilo. Vikosi vya amani vya Umoja wa Mataifa,sasa vimeimarishwa kwenye eneo hilo la mvutano katika mpaka wa Lebanon na Israel.Wakati huo huo serikali ya Israel imeionya Lebanon kuwa haitostahmili vitendo vyo vyote vya uadui dhidi ya vikosi vyake.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com