1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Vikosi vya Lebanon vimepambana na wanamgambo

20 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC0N

Mapigano yamezuka kati ya vikosi vya serikali ya Lebanon na wanamgambo walio na makao yao katika kambi ya wakimbizi wa Kipalestina,katika mji wa Tripoli ulio kaskazini mwa nchi.Duru za kijeshi za Lebanon zimesema,wanajeshi wake 7 wameuawa katika mapigano hayo,ikiaminiwa kuwa wanamgambo hao wana mahusiano na Syria.Duru hizo zikaeleza kuwa wanajeshi 3 waliuawa na 4 walijeruhiwa katika kambi ya wakimbizi ya Nahr al-Bared,karibu na mji wa bandari wa Tripoli.Wengine 4 waliuawa baada ya wanamgambo kushambulia kikosi kilichokuwa kikipiga doria katika eneo la kaskazini la Koura.Kwa mujibu wa duru hizo za kijeshi,vikosi vilipambana na wanamgambo wa kundi la Fatah al-Islam,ambalo maafisa wa Lebanon wanaamini linafanya kazi za upelelezi kwa niaba ya Syria.