BEIRUT: Majeshi ya Lebanon yakabiliana tena na Fatah al-Islam | Habari za Ulimwengu | DW | 02.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BEIRUT: Majeshi ya Lebanon yakabiliana tena na Fatah al-Islam

Majeshi ya Lebanon yamewazingira kwa mara nyingine tena wanamgammbo wa Kiislamu waliojificha kwenye kambi ya wakimbizi wa Kipalestina karibu na mji wa Tripoli.

Milipuko ilikuwa ikisikika leo asubuhi, siku moja baada ya watu kumi na tisa wakiwemo wanajeshi wawili wa Lebanon kuuawa kwenye mapigano katika kambi ya Nahr al-Bared.

Waziri wa mawasiliano, Marwan Hamadeh amewaambia waandishi wa habari kwamba majeshi ya nchi hiyo yamepania kukabiliana vilivyo na wanamgambo hao wanaosemekana wana uhusiano na mtandao wa al-Qaeda.

Waziri Marwan Hamadeh amesema:

"Tumeamua kukabiliana na Fatah al-Islam, kundi ambalo limeteka kila kilichobaki kambini. Mara hii majeshi yetu yamejitolea kidhati kuwafagilia mbali wanamgambo wa Fatah al-Islam"

Majeshi ya Lebanon yamewataka wanamgambo hao kujisalimisha na pia yamewatolea wito wakazi wa kambi hiyo kutowapa hifadhi wanamgambo hao.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com