1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING:Kansela Angela Merkel akutana na viongozi wa China

27 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBVa

Kansela Angela Merkel ameanza mazungumzo na viongozi wa China hii leo mjini Beijing.Kabla hajakutana na waziri mkuu wa China Wen Jiabao Kansela aliusifu uhusiano kati yake na waziri mkuu huyo.

Akiwasili China hapo jana alisema

Miongoni mwa masuala atakayoyajadili na viongozi wa nchi hiyo ni pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa,haki za binadamu na ushirikiano wa kiuchumi miongoni mwa masuala mengine. Katika ziara hiyo ya siku tatu Merkel amepangiwa pia kuwa na mazungumzo na rais Hu Jintao na anatarajiwa kukutana na makundi ya kitamaduni nay ale ya kutetea haki za kibinadamu.

Hapo jana China imekanusha habari kwamba raia wake wanaohusika jeshini walikuwa na dhamana ya kuweka virusi mitambo ya Komputa inayotumiwa na serikali ya Ujerumani suala ambalo pia ni nyeti katika ziara hii ya Merkel nchini Japan na China.

Gazeti la kila wiki la Ujerumani Der Spiegel liliripoti katika makala yake ya jumapili kwamba mawakala wa usalama nchini Ujerumani waligundua kwamba Komputa zinazotumika katika ofisi za kansela na wizara tatu nyingine zilikuwa na programu za upelelezi kutoka China.Jumatano Kansela atakwenda japan kukutana na viongozi wa nchi hiyo.