Beijing.China yafungua huduma za bure za Ukimwi. | Habari za Ulimwengu | DW | 09.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Beijing.China yafungua huduma za bure za Ukimwi.

Kituo cha kwanza cha afya kitakachotoa huduma za Ukimwi bila ya malipo nchini China kimefunguliwa katika mji mkuu Beijing, ikiwa ni dalili ya kuvumilia na kufahamu maradhi hayo yanayozidisha matatizo katika jamii.

Kituo hicho cha afya kinatoa huduma za bure za uangalizi na matibabu kwa watu walioambukizwa virusi vya ukimwi na maradhi mengine yanayoambukizwa kwa njia za kujamiiana.

Mashirika kadhaa yanayojishughulisha na kupambana na maradhi ya ukimwi pamoja na yale ya kupambana na vitendo vya kujamiiana kwa jinsia moja yanaendelea kutoa shutma zao nchini kote.

Hata hivyo wagonjwa wanatibiwa katika kituo hicho bila ya kutaja majina yao.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com