1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAVARIA: Rais Putin amaliza ziara rasmi nchini Ujerumani

Rais Vladmir Putin wa Urusi amemaliza ziara yake rasmi nchini Ujerumani kwa kulitembelea jimbo la Bavaria ambapo alikutana na wafanyabiashara pamoja na viongozi wa serikali.

Rais Putin amesisitiza nia ya nchi yake juu ya kuekeza vitega uchumi katika makampuni ya Ujerumani.

Waziri Mkuu wa jimbo hilo la Bavaria bwana Edmund Stoiber amesema kuwa Ujerumani ipo tayari kushirikiana na Urusi katika sekta za uchumi na tekinolojia.

Katika ziara yake ya siku mbili nchini Ujerumani rais Putin alijaribu kutafuta msaada na ushirikiano wa kuingiza usasa katika uchumi wa Urusi, unaostawi kwa haraka.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com