BAGHDAD:Marekani yajiweka mbali na kunyongwa Saddam | Habari za Ulimwengu | DW | 04.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD:Marekani yajiweka mbali na kunyongwa Saddam

Marekani imejiweka mbali na jinsi kiongozi wa zamani wa Iraq Saddam Hussein alivyongwa.

Kamanda wa kikosi cha marekani nchini Iraq, Meja Generali William Caldwell, akizungumza mjini Baghdad amesema kuwa kunyongwa kwa Saddam kulifanywa na serikali ya Iraq.

Hatua hiyo imekuja huku kukiwa na shutuma kutoka kwa jamii ya wasunni jinsi Saddam alivyodhalilishwa na washia kwa maneno ya kashfa kabla ya kunyongwa kwake.

Serikali ya Iraq imeanzisha uchunguzi kumtafuta mtu aliyerekodi tukio la kunyongwa kwa Saddam kwa kutumia simu ya mkononi, ambapo tayari walinzi wawili wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo.Walinzi hao walikuwa miongoni mwa wale waliyokuwa katika tukio la kunyongwa Saddam

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com