1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Watu tisa wauwawa na wengine watekwa nyara.

12 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCtg

Kiasi watu tisa wameuwawa na wengine kadha wametekwa nyara baada ya watu wenye silaha kuvamia mabasi madogo matatu kusini mwa mji mkuu wa Iraq , Baghdad.

Polisi wamesema kuwa wengi wa wahanga ni Washia. Hapo mapema , mabomu kadha katika magari yamewauwa watu wanane na kuwajeruhi wengine kiasi cha 40 katika mji huo mkuu.

Wakati huo huo , majenerali wa ngazi ya juu wa Marekani wameanza kufikiria upya mkakati wao wa kijeshi nchini Iraq.

Mjini Washington , Jenerali Peter Pace, ambaye ni mwenyekiti wa wakuu wa majeshi mbali mbali ya nchi hiyo, amesema kuwa kutakuwa na mabadiliko makubwa kufuatia kujiuzulu kwa waziri wa ulinzi Donald Rumsfeld, ambaye amejiuzulu siku ya Jumatano.